Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Alireza Arafi katika kikao cha mashauriano na viongozi wa idara ya wakfu na rasilimali endelevu za Hawza za kielimu nchini Iran, kilichofanyika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Hawza za kielimu katika mji wa Qom Iran, alisisitiza umuhimu wa nafasi na majukumu makubwa ya Hawza katika zama za sasa, pamoja na ulazima wa kuungwa mkono kwa njia zote taasisi hii takatifu.
Hali ya sasa ya Hawza na ulazima wa uungwaji mkono mpana
Mkurugenzi wa Hawza za kielimu akisema kuwa hali ya Hawza leo imebadilika kimsingi ikilinganishwa na miaka hamsini iliyopita, alisema: Hali ambayo Hawza na wanazuoni wa dini wanakabiliana nayo leo ni nyeti sana, na majukumu yaliyopo mbele yao ni mengi na yenye sura mbalimbali. Nafasi hii nyeti inahitaji uungwaji mkono mpana ambao lazima uzingatiwe na wafadhili pamoja na jamii kwa ujumla.
Ayatollah Arafi huku akisisitiza kwamba majukumu ya leo ya Hawza hayawezi kulinganishwa na ya zamani, alisema: Matarajio na majukumu ya Hawza leo hayawezi kabisa kulinganishwa na ya miaka hamsini iliyopita. Pamoja na shughuli zote tunazofanya ndani ya Hawza, huenda tunatekeleza chini ya asilimia moja ya majukumu yaliyo mabegani mwetu.
Kulinganisha Hawza kabla na baada ya Mapinduzi; kutoka upweke hadi mahitaji ya kimataifa
Mkurugenzi wa Hawza za kielimu, huku akirejelea kipindi cha masomo yake kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu, alieleza mazingira yenye mipaka ya wakati huo na kusema: Hawza kabla ya Mapinduzi ilikuwa imejikita katika shule chache na idadi ndogo ya watu, na mahitaji ya kimataifa hayakuwepo kama yalivyo leo. Bila shaka, wanazuoni wakubwa wa kipindi hicho kama Allama Tabataba’i, Shahid Mutahhari na wengine walifanya juhudi kubwa zenye thamani.
Mapinduzi ya Kiislamu na kupanuka majukumu kwa kiwango kisichokuwa na mfano
Aliongeza kuwa: Leo hali imebadilika kabisa, na dunia — kwa uwepo wa mitandao ya mawasiliano — imekuwa ngumu mara elfu zaidi kuliko miaka hamsini iliyopita. Milango ya dunia imefunguliwa kwa mafundisho ya Ahlul-Bayt (as), na mahitaji ya kimataifa katika mafundisho haya yameongezeka kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.
Mahitaji makubwa ya kimataifa
Ayatollah Arafi aliendelea kusema: Mimi, kama mtu aliyekuwepo kwa muda wa miaka arobaini katika taasisi na mifumo ya Hawza, ninaamini kwamba kile ambacho Hawza inacho leo hakitoshelezi hata asilimia moja ya mahitaji na majukumu yake makubwa. Mahitaji ya dunia kwenye dini ya Mwenyezi Mungu na mafundisho ya Uislamu leo ni makubwa zaidi kuliko uwezo wetu wa sasa, na utekelezaji wa majukumu haya unahitaji uungwaji mkono wa pande zote.
Kuenea kwa Ushia duniani ni matokeo ya baraka ya Mapinduzi ya Kiislamu
Mjumbe wa wanazuoni wa Baraza la Walinzi wa Katiba alisisitiza kuwa: Leo mafundisho ya Uislamu na Ushia yanaenezwa katika takribani nchi 180 duniani na wanazuoni waliopata mafunzo baada ya Mapinduzi ya Kiislamu wamepata mafanikio ambayo hayakuwepo kabla ya Mapinduzi. Aliongeza kuwa: Sasa karibu katika nchi zote za dunia, yaani katika nchi takribani 170 hadi 180, mafundisho ya Uislamu halisi na Ushia yanaenezwa na wanazuoni waliobobea na kulelewa baada ya Mapinduzi. Jambo hili halikuwa na mfano kabla ya Mapinduzi, na yote haya ni kwa baraka ya Mapinduzi na uwepo wa watu.
Nafasi ya msingi ya taifa la Iran katika ushindi na kuendelea kwa Mapinduzi
Ayatollah Arafi alisisitiza: Mapinduzi na mafanikio yake ni ya taifa la Iran. Ni watu waliokuwa mstari wa mbele. Kama tusingekuwa na matukio ya kihistoria kama 19 Dey, 12 Bahman na 22 Bahman, njia hii isingetimia. Watu wa Iran, baada ya maelfu ya miaka, waliinua bendera ya Uislamu duniani kote. Aliendelea kusema: Kwa mara ya kwanza katika historia, katika zaidi ya nchi mia moja duniani, dhana kama Ashura, Mahdawiyya, Intidhar na Ushia zimewasilishwa na kufanywa kuwa sehemu ya mazingira ya jamii hizo.
Mkurugenzi wa Hawza za kielimu alitathmini pia shughuli za taasisi za Hawza katika uwanja wa kimataifa na kusema: Pamoja na shughuli zote zilizofanywa ndani ya Hawza, Jamiat al-Mustafa al-Alamiyya na taasisi nyingine zinazohusiana, tumefanikisha kufikia sehemu ndogo tu ya mahitaji ya kimataifa.
Kufunguka kwa upeo wa kimataifa
Ayatollah Arafi alisisitiza: Kwa baraka ya damu ya mashahidi, Mapinduzi ya Kiislamu, na uungwaji mkono wa wafadhili na wananchi, upeo wa kipekee umefunguliwa mbele yetu duniani, na mataifa yamesimama imara juu ya maadili ya Kiislamu.
Hakuna haja ya silaha; Nahj al-Balagha na Sahifa Sajjadiyya ni nguvu laini ya Iran
Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza alisema: Mwanafunzi anayechukua hatua kwa ikhlasi anaweza kuwasilisha ujumbe wa Ushia na mafundisho ya kina kama Nahjul-Balagha na Sahifa Sajjadiyya kwa walimwengu. Hili ndilo linalowatia hofu maadui wetu — maana ikiwa hawatuzuia, hatutahitaji silaha wala makombora. Ayatollah Arafi alisisitiza: Dunia inaelewa siku baada ya siku kwamba sisi hatuna nia ya vita, bali ni wabebaji wa ujumbe wa Nahjul-Balagha na Sahifa Sajjadiyya.
Mapokezi ya kimataifa kwenye Mahdawiyya na mafundisho ya dini
Akirejelea suala la Mahdawiyya na Intidhar, alisema: Watu duniani wanapokea kwa hamasa kubwa sana maelezo kuhusu Mahdawiyya na mafundisho ya Ahlul-Bayt (as). Huu ni uwanja mpana sana unaohitaji kufanyiwa kazi zaidi.
Mjumbe wa wanazuoni wa Baraza la Walinzi wa Katiba alieleza pia; majukumu mazito ya Hawza mbele ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na akirejelea nyaraka za juu na maelekezo ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, alichora mafaili makuu matatu mbele ya watafiti na wanazuoni wa Hawza.
Ulazima wa kuzalisha elimu ya kijamii ya Kiislamu ili kujaza pengo la kisheria
Mkurugenzi wa Hawza za kielimu alisema: Kabla ya Mapinduzi hapakuwa na nyaraka, sheria na kanuni zilizojengwa juu ya Uislamu. Lakini leo, kwa kuwa mfumo unaoitwa Uislamu umejengwa, maelfu ya mahitaji mapya yamejitokeza, na kuyatekeleza ni jukumu la Hawza. Tumetambua sehemu ndogo tu ya mahitaji haya na tunaendelea kuyarekebisha.
Maoni yako